ZINAZOVUMA:

Wavuvi ruksa kuuza samaki popote – Waziri Mkuu

Waziri Mkuu Kassim majaliwa amewapa ruhusa wavuvi wa samaki na...

Share na:

Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassimu Majaliwa, amesema wavuvi wa samaki na dagaa wanaruhusiwa kuuza kwenye mwalo ama soko lolote nchini na hakuna halmashauri itazuia.

Amesema hayo wakati akizungumza na wavuvi na wafanyabiashara wa samaki na dagaa, mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika soko la kisasa la mazao ya samaki mwalo wa Chato.

Na kuongeza kuwa uamuzi huo umekuja baada ya baadhi ya halmashauri ikiwemo ya Chato kata ya Muganza na Mleba kuna mvutano kugombania wavuvi, hali iliyoathiri maendeleo ya shughuli za uvuvi.

“Tumewaambia hakuna kuwazuia wavuvi kuuza samaki popote, mvuvi anayo fursa ya kupeleka samaki popote, hata kama baharini (ziwani) ni kandokando yako,” amesema.

Amesema kuwa serikali imejizatiti kuboresha mialo yote nchini, ili kukuza sekta ya uvuvi kupitia ujenzi wa maeneo ya kisasa ya kuhifadhi na kuuza samaki kwa wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi.

Amewaomba Watanzania kuchangamkia fursa ya uvuvi, kwa kuanzisha kuanzisha vikundi ili wanufaike na mpango wa uwezeshaji kiuchumi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu na halmashauri.

Tayari ofisi yake imekuja na mpango wa kuikusanya na kuiweka pamoja mifuko yote inayotoa mikopo, ili iwe rahisi kwa wananchi kuifikia.

Ameelekeza ofisi ya mkurugenzi wa halmashauri kusimamia uundaji vikundi na utoaji elimu kwa wavuvi, ili waweze kukopesheka na kuendesha shughuli zao kibiashara zaidi.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato, Mandia Kihiyo amesema mradi wa mwalo wa kisasa umegharimu Sh bilioni 1.7 na utanufaisha wafanyabishara wa samaki wapatao 1,120.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya