ZINAZOVUMA:

TMA: Kimbunga “IALY” kusababisha mvua na upepo

Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini Tanzania (TMA) yatangaza uwepo...

Share na:

Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini Tanzania (TMA) imesema kuwa, kimbunga “IALY”, kinachoendelea kuvuma kaskazini mwa Madagascar ambapo mwanzo kilitabiriwa kuishia baharini kinawez sababisha mvua na upepo nchini.

Kimbunga hicho kilitabiriwa kuisha kabla ya kufika nchi kavu, ila Mamlaka hiyo imebadilisha na kusema kuwa kimbunga hicho kinaweza kusababisha mvua kubwa na upepo mkali nchini siku ya jumanne ya 21 Mei 2024.

Taarifa hiyo ilitolewa ikisema kuwa kimbunga hicho kipo umbali wa kilomita 680 kutoka pwani ya Tanzania, na kinatarajiwa kusababisha mvua kubwa, upepo mkali wa zaidi ya kilomita 40 kwa saa na mawimbi yanayozidi mita 2, huku mvua kubwa ikitabiriwa kunyesha katika maeneo ya pwani hadi jumatano ya Mei 22 2024.

Endelea Kusoma

Waziri Mkuu wa Slovakia aonekana kwenye hotuba yake kupitia mitandao wiki 3

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya