Spika wa Bunge, Dkt Tulia Ackson ni miongoni wa wabunge waliowasilisha maombi ya kugawa majimbo yao ili kuwa mawili kutokana na ukubwa na wingi wa watu.
Taarifa hiyo imetolewa leo bungeni na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Ummy Nderiananga wakati akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Viti Maalum Sophia Mwakagenda.
Katika swali lake Mwakagenda ameuliza ni lini serikali italigawa jimbo la Mbeya mjini ambalo linaongozwa na Spika wa Bunge Tulia Ackson kutokana na ukubwa wake.
“Mheshimiwa Tulia Ackson alishawasilisha kwenye mamlaka nia ya kuomba jimbo hilo ligawanywe, serikali inatafakari maombi hayo na wakati utakapofika vigezo vitatazamwa,”