ZINAZOVUMA:

Raisi Samia atoa ajira za elimu na afya.

Raisi Samia kupitia wizara ya nchi OR- TAMISEMI ametoa ajira...

Share na:

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan ameridhia kutoa kibali cha kuajiri watumishi 21,200 wa Kada za ualimu na Afya.

Hayo yamesemwa leo tarehe 12 Aprili 2023 na waziri wa Nchi- OR TAMISEMI Angellah Kairuki wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Idadi ya watumishi watakaoajiliwa katika Kada za Ualimu ni 13,130 ambao watafundisha katika shule za Msingi na Sekondari.

Aidha, idadi ya watumishi watakoajiliwa katika kada za Afya ni 8,070 ambao watafanya kazi katika Hospitali za Halmashauri, Vito vya Afya na Zahanati.

Endelea Kusoma

Kijana Edward awebwa ahukumiwa miaka 6 jela nchini Uganda, kwa kumtukana rais

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya