ZINAZOVUMA:

Urusi inapambana kulipa fadhila kwa Iran

Shirika la Gazprom limeshindwa linaendelea mpango wa bomba la gesi...

Share na:

Taifa la Urusi linalosifika kwa kuzalisha gesi kwa wingi na kusambaza gesi Ulaya, inaenelea na mpango wake wa kupeleka gesi nchini Iran ili kulipa fadhila kwa nchi hiyo.

Nchi ya Urusi ambayo bado inaendelea na mapigano dhidi ya Ukraine, imekuwa ikipokea ndege ndogo za kivita zisizo na rubani “drones” kutoka Iran.

Hata hivyo katika jitihada za kutaka kulipa fadhila Urusi iliweka azma ya kupeleka gesi Iran kwa njia ya bomba.

Ingawa hadi sasa jitihada hizo hazijazaa matunda kutokana na vikwazo vya ujenzi wa bomba vilivyotokea kutokana na kutokana ridhaa ya nchi ya Turkmenistan iliyopo katika njia ya bomba hilo.

Kikwazo hicho kimekuja baada ya shirika la gesi (Gazprom) la Urusi kuingia Makubaliano ya kimkakati na Shirika la Gesi la Iran (NIGC), wakikubaliana Gazprom kupeleka gesi nchini Iran kupitia Turkmenistan.

Ramani ya Eurasia
Ramani ya ukanda wa Eurasia ikionesha nchi za ukanda huo

Endelea Kusoma

Kijana Edward awebwa ahukumiwa miaka 6 jela nchini Uganda, kwa kumtukana rais

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya