ZINAZOVUMA:

Hospitali ya Rufaa Chato kutoa huduma za Moyo

Wizara ya Afya imeazimia kuifanya Hospitali ya Rufaa ya Chato...

Share na:

Serikali kupitia Wizara ya Afya imedhamiria Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Chato kuwa kituo cha umahiri wa matibabu ya ubingwa na ubingwa bobezi wa moyo.

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema hayo leo Machi 16, 2024 wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya Ukimwi ikiongozwa na mwenyekiti wake, Stanslaus Nyongo kukagua miradi ya ujenzi wa jengo la wodi la ghorofa mbili pamoja na jengo la kutakasia vifaa yanayojengwa katika hospitali hiyo.

“Kanda ya Ziwa ina watu karibu milioni 22, hivyo tukaona kuna haja ya kuwa na Hospitali ya Rufaa ya Kanda nyingine katika ukanda huu wa ziwa na ianze kutoa huduma za matibabu ya ubingwa na ubingwa bobezi wa moyo katika ukanda huo wa ziwa ili waweze kusaidiana na Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando,” amesema Ummy.

“Waziri Ummy amesema kesi za magonjwa ya moyo za watu wa Kanda ya Ziwa (Mwanza, Geita, Simiyu, Shinyanga, Kagera pamoja na Kigoma) wanataka ziishie Chato ili kurahisisha upatikanaji wa huduma hizo karibu na wananchi wa Kanda ya Ziwa pamoja na kupunguza msongamano wa wagonjwa wa moyo JKCI – Dar es Salaam,”ameongeza Ummy.

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,