ZINAZOVUMA:

AngloGold kuhama soko la hisa na makao makuu

Wanahisa wa AngloGold ashanti waridhia maombi ya kuhama soko la...
Nembo ya angloGold Ashanti

Share na:

Uongozi wa Kampuni ya makini ya Anglogold Ashanti (ANG:JNB) umepitisha maamuzi ya kubadili soko la hisa la msingi kutoka Johannesburg (JSE), Afrika Kusini, na kuiorodhesha katika soko la hisa la New York (NYSE) nchini marekani kama soko la msingi.

Kampuni hiyo imefikia uamuzi huo siku Ijumaa baada ya wanahisa wakuu kupitisha uamuzi huo kwa asilimia 98.

Kampuni hiyo imeorodheshwa katika masoko ya hisa manne Johannesburg, New York, Ghana na Australia.

Mbali na uamuzi huo wa kuhamisha soko la hisa, pia wanahisa wa Anglogold wamepitisha maamuzi ya kuhamisha makao mkuu ya kampuni hiyo kutoka Johannesburg hadi London, Uingereza.

Sababu kuu iliyosukuma kampuni hiyo kuhama soko la hisa ni kutarajia fedha zaidi za uwekezaji katika dhahabu.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya