ZINAZOVUMA:

Sheikh Ali Basaleh kuzikwa leo

Mwili wa marehemu Sheikh Ali Basaleh utaswaliwa baada ya swala...

Share na:

Mwanazuoni na sheikh maarufu Maalim Ali Basaleh amefariki dunia jana Jumapili katika Hospitali ya Aga Khan alipokuwa akipatiwa matibabu akisumbuliwa na matatizo ya figo na saratani.

Mtoto wa marehemu Abdullatif Ali Basaleh amesema baba yake amefariki jana saa 12 jioni baada ya kulazwa kwa takribani wiki mbili na nusu akipatiwa matibabu hayo.

Sheikh Ali Basaleh aliwahi kuwa imamu wa msikiti wa Idrissa uliopo kariakoo.

Mwili wa marehemu Sheikh Ali Basaleh utaswaliwa leo baada ya dhuhur katika msikiti wa mtoro kariakoo na kisha kwenda kuzikwa katika makaburi ya kisutu.

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya