ZINAZOVUMA:

Urusi yawafukuza wanadiplomasia wa Marekani

Wizara ya Mambo ya Nje nchini Urusi imetoa siku saba...

Share na:

Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi imewapa siku saba wanadiplomasia wa ubalozi wa Marekani nchini Urusi wawe wameshaondoka.

Wizara hiyo imewataja Jeffrey Sillin na David Bernstein kama watu wasiofaa na hawatakiwi kuwepo nchini humo haraka iwezekanavyo.

Wizara hiyo imesema kuwa watu hao walifanya shughuli haramu na kushirikiana na mfanyakazi wa zamani wa Ubalozi Mkuu wa Marekani huko Vladivostok, Robert Shonov, ambaye Urusi ilimshtaki kwa vitendo vya kihaini.

Robert Shonov alifanya kazi katika Ubalozi wa Marekani huko Vladivostok kwa zaidi ya miaka 25 hadi Urusi ilipoamuru kufukuzwa kwa wafanyikazi wa misheni ya Marekani mnamo 2021.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya