ZINAZOVUMA:

Siku tatu za maombolezo baada ya kupoteza askari 29 Niger

Uongozi wa kijeshi nchini Niger umetoa siku tatu za maombolezo...

Share na:

Wizara ya Ulinzi nchini Niger imesema wanajeshi 29 wameuawa katika shambulio lililofanywa na watu wanaoshukiwa kuwa waasi magharibi mwa nchi hiyo huku siku tatu za maombolezo zikitangazwa.

Shambulio la aina hiyo limetajwa kuwa baya zaidi tangu jeshi lilipochukua mamlaka katika mapinduzi ya kijeshi yaliyofanyika mwishoni mwa Julai mwaka huu.

Katika taarifa iliyorushwa kwa njia ya televisheni maofisa walisema wanajeshi hao walikuwa wakilengwa na zaidi ya wanamgambo 100, wakitumia silaha ikiwa ni pamoja na vilipuzi vya kujitengenezea.

Siku tatu za maombolezo ya kitaifa zimetangazwa huku mashambulizi kutoka wanajihadi dhidi ya jeshi yakiongezeka tangu lilipofanya mapinduzi na kuchukua mamlaka ili kuweza kupambana vyema na wanamgambo.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya