ZINAZOVUMA:

Ndege ya mizigo ya ATCL sasa mambo mazuri

Ndege ya mizigo ya Shirika la ndege nchini ATCL imefanya...

Share na:

Ndege ya mizigo ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) leo Jumatatu, Julai 10, 2023 inatarajia kufanya safari yake ya pili ya kupeleka mzigo Dubai huku ikiendelea kuvutia kasi masoko mengine muhimu.

Julai 7, 2023 ndege hiyo aina ya Boeing 767-300F ilifanya safari yake ya kwanza kwenda Dubai ikitokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Julius Nyerere (JNIA).

Mkurugenzi wa Biashara wa Kampuni hiyo, Patrick Ndekena alisema ratiba ya safari za Dubai itakuwa mara mbili kwa wiki ambayo itakua ni Ijumaa na Jumatatu.

Aidha alisema adhma ya ATCL ni kuhakikisha bidhaa za wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi zinafika kwa wakati na zikiwa na ubora wake kwenye nchi mbalimbali kwa kadri ya inavyotakiwa.

Endelea Kusoma

Waziri Mkuu wa Slovakia amejeruhiwa vibaya katika jaribio lakutaka kumuua kwenye mji

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya