ZINAZOVUMA:

Bwawa sio sababu ya Mafuriko Rufiji na Kibiti

Shirika la umeme TANESCO limekanusha kuwa Bwawa la Nyerere ndio...

Share na:

Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) limefafanua kuwa mradi wa bwawa la umeme la Julius Nyerere (JNHPP) umechangia kupunguza athari za mafuriko katika wilaya ya Rufiji na Kibiti.

Tofauti na kinyume chake inavyoripotiwa kuwa mradi huo umechangia kutokea kwa mafuriko hayo yanayoendelea maeneo hayo.

Taarifa ya kurugenzi ya mawasiliano na uhusiano kutoka TANESCO makao makuu, imeeleza kuwa maeneo hayo yamekuwa yakikumbwa na mafuriko kwa miaka mingi ya nyuma.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa athari za mafuriko kwa Sasa zinaonekana zimechangiwa kwa kiasi kikubwa na mvua za El-nino, ambazo hadi sasa bado zinazoendelea kunyesha hivyo kusababisha mafuriko katika maeneo mbalimbali nchini.

“TANESCO Inakanusha taarifa zozote za upotoshaji zinazohusisha bwawa la Julius Nyerere na mafuriko ya Kibiti na Rufiji”.

Pia taarifa ya shirika hilo imekemea upotoshaji unaofanywa na baadhi ya watu wasio na Nia njema, kubeza juhudi za serikali katika kuimarisha hali ya upatikanaji umeme nchini.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya