ZINAZOVUMA:

Bwawa la Mwl Nyerere halitapunguza gharama za umeme

Kukamilika kwa bwawa la kuzalisha umeme la Julius Nyerere hakutapunguza...

Share na:

Licha ya gaharama za uzalishaji wa umeme kutarajiwa kushuka baada ya kukamilika kwa Bwawa la kuzalisha umeme la Julius Nyerere (JNHPP) Juni 2024, imebainika kuwa uzalishaji huo hautapunguza bei ya umeme kwa wateja.

Bwawa hilo linatarajia kuzalisha megawati 2,115 za umeme zitakazoingizwa katika Gridi ya Taifa.

Hayo yameelezwa leo Julai 27 na Mkurugenzi wa Tanesco, Maharage Chande katika kikao kazi kati ya Tanesco na Msajili wa Hazina na wahariri wa vyombo vya habari lengo kuelezea mafanikio na kazi za shirika hilo.

Amesema kwa mwaka 2020/2021 gharama ya uzalishaji wa umeme ulikuwa Sh1.5 trilioni ikilinganishwa na ongezeko la Sh 1.6 trilioni kwa mwaka 2021/2022.

“Mradi wa Mwalimu Nyerere ukikamilika gharama za umeme zitashuka lakini hatutashusha bei kwasababu tutashindwa kwenda,” amesema.

Endelea Kusoma

Kijana Edward awebwa ahukumiwa miaka 6 jela nchini Uganda, kwa kumtukana rais

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya