ZINAZOVUMA:

Maelfu waathirika na mafuriko kilosa

Zaidi ya watu elfu moja na mia nne wameathirika kwa...

Share na:

Watu 1, 404 wameathirika na mafuriko ya mvua zinazoendelea kunyesha katika Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro huku nyumba 351 zikijaa maji.

Pia, vyoo 368 vimebomoka na kaya 368 zikiathirika.

Hayo yalisemwana Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Shaka Hamdu Shaka, alipotembelea waathirika hao.

Shaka amesema Kitongoji cha Kampala kaya 161 na watu 624 wameathirika, Kitongoji cha Madizi kaya 137 na watu 531 wakati Kitongoji cha Estate kaya zilizoathirika ni 57 na watu 196.

Kitongoji kingine ni cha Lugunga kata nane na watu 32 wameathirika, Kitongoji cha PWD kaya tano na watu 20 wameathirika.

Shaka amesema nyumba zilizobomoka ni 17 tano zinatoka Kitongoji cha Kampala, nyumba nane Kitongoji cha Estate na nyumba nne Kitongoji cha Madizini.

“jumla ya vyoo 368 vimeathirika kutokana na mafuriko, hivyo kufanya maji kuwa machafu baada ya vyoo hivyo kutapishwa na mafuriko baada ya kubomoka,” amesema Shaka.

Aidha, amesema jumla ya visima 30 vya maji vinavyotumika vimeathirika na mafuriko hayo kwa kuingiliwa na maji machafu.

Akizungumzia kuhusina na hali ya miundombinu ya barabara, Shaka amesema zaidi kilometa 170 za barabara zimeathirika kwa maji kukata barabara na kusababisha kukatika kwa mawasiliano baina ya Kilosa na Mikumi maeneo mengine ya yanayounganisha vijiji na vijiji hali iliyosababisha usumbufu mkubwa kwa wananchi na shuhuli za usafirishaji bidhaa.

Amesema Machi 17 mwaka huu maji mengi yalijaa katika mto Miyombo unaopita katika vijiji vya Ulaya, Zombo na Changarawe baada ya mvua kubwa kunyesha katika vijiji vya Kisanga, Madizini na Kitunduweta.

Pia amesema kijiji cha Changarawe kimekuwa na matukio ya kupatwa na mafuriko mara kwa mara tangu mwaka 2016 na msimu huu wa mvua tangu Desemba mwaka jana hadi sasa ni tukio la tisa la mafuriko.

Endelea Kusoma

Waziri Mkuu wa Slovakia amejeruhiwa vibaya katika jaribio lakutaka kumuua kwenye mji

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya