ZINAZOVUMA:

Shule ya Kivukoni A Ulanga yafungwa sababu ya mafuriko

Mkuu wa Wilaya ya Ulanga Dkt. Julius Ningu asimamisha masomo...

Share na:

Shule ya msingi kivukoni A Iliyopo kata ya Minepa wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro imefungwa kwa siku 15 baada ya kukumbwa na mafuriko

Ameeleza hayo Mkuu wa wilaya ya Ulanga Dk. Julius Ningu wakati akifanya tathmini ya maafa hayo na kusema kuwa uamuzi ambao umechukuliwa ni kwa lengo la kuzingatia usalama wa wanafunzi na walimu

Aidha Dk. Ningu amesema kwa upande wa miundombinu bado usafiri wa barabara ni changamoto baada ya barabara kuu kutoka Ifakara kwenda Ulanga na zandani kuharibika na nyingine kushindwa kupitika kwa kujaaa maji

“Tumefunga shule jana baada ya kuona hali sio nzuri pamoja na kwamba tumeweka siku 15 hata hivyo tutaangalia na hali ya hewa kama mvua zitaendelea basi itabidi tuwahamishie wanafunzi kwenye shule ya msingi Kivukoni B” amesma Dk. Ningu

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,