ZINAZOVUMA:

Wawili wafariki ajali ya malori Njombe

Ajali ya Lori la Mbao na lori la Makaa ya...

Share na:

Watu wawili wamefariki dunia baada ya gari lao kupinduka, eneo la Lihogosa katika Halmashauri ya wilaya ya Wanging’ombe Mkoani Njombe.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe Mahamoud Banga amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo Aprili 19, 2024.

Kamanda Banga ameeleza chanzo cha ajali hiyo kuwa Lori la mbao lilikwaruzana na Lori la makaa ya mawe na kupinduka, likiwa linatokea makambako kuelekea Songea.

“Dereva wa lori la mbao alipoteza maisha papo hapo pamoja na mmiliki wa mzigo, lakini utingo wa lori ni majeruhi na amelazwa hospitali ya Rufaa ya Njombe”.

Na kuongezea kuwa “Mpaka sasa dereva wa lori la makaa ya mawe bado hajakamatwa ili ahojiwe kuhusu ajali hiyo”.

Chanzo: Mwananchi

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya