ZINAZOVUMA:

Rais aliyepinduliwa Gabon aruhusiwa kusafiri nje ya nchi

Raisi aliyepinduliwa nchini Gabon Ali Bongo ameachiliwa na kuruhusiwa kusafiri...

Share na:

Rais wa mpito na kiongozi wa mapinduzi wa Gabon, Jenerali Brice Nguema ametoa ruhusa kwa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo, Ali Bongo kusafiri nje ya nchi baada ya kukaa kizuizini kwa zaidi ya wiki moja.

“Ana uhuru wa kutembea… na anaweza kusafiri nje ya nchi akitaka,” Jenerali Brice Nguema amesema katika taarifa iliyosomwa kwenye runinga ya serikali jana usiku Septemba 6, 2023.

AFP imeripoti kuwa Bongo, aliyekuwa madarakani kwa miaka 14, alikuwa chini ya kizuizi cha nyumbani tangu mapinduzi ya kijeshi ya Agosti 30, 2023; yaliyotekelezwa bila umwagaji damu baada ya Tume ya Uchaguzi kutangaza kuchaguliwa kwake tena katika uchaguzi unaotajwa kuwa na udanganyifu.

“Kwa kuzingatia hali yake ya afya, Rais wa zamani wa Jamhuri, Ali Bongo ana uhuru wa kutembea. Anaweza kusafiri nje ya nchi ikiwa anataka kufanya uchunguzi wake wa afya,” Kanali Ulrich Manfoumbi Manfoumbi amesema, wakati akisoma taarifa kwa vyombo vya habari iliyotiwa saini na Nguema ambaye alikula kiapo chake kama Rais wa mpito siku ya Jumatatu Septemba 4 mwaka huu.

Bongo alishikwa na ugonjwa wa kiharusi mnamo Oktoba 2018; ambacho kilimfanya adhoofike kimwili, na hivyo kujikuta akipata shida hasa anapotaka kusogeza mguu na mkono wake wa kulia.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya