ZINAZOVUMA:

Ajali yafunga barabara ya Morogoro

Ajali ya Lori maeneo ya Viwagza yasababisha foleni iliyofunga barabara...

Share na:

Ajali ya gari iliyotokea maeneo ya vigwaza karibu na mizani imesababisha foleni kubwa katika barabara hiyo. Ajali hiyo imesababisha gari zote zinazotoka Dar es salaam kukwama hapo kwa saa kadhaa.

Huku barabara za kwenda na kurudi morogoro ikiwa imejaa magari yatokayo Dar. Magari machache yanayotoka Chalinze kuja Dar yanapita kila baada ya muda.

Hali hii imesababisha foleni kwa magari ya mikoani, ya mizigo na hata daladala za mbezi kwenda Chalinze na msata. Pamoja na kuwa tayari gari iliyosababisha ajali hiyo kutolewa bado watu mbalimbali wanasaidia kufungua njia kwa kuelekeza magari ambayo tayari yalishaweka msongamano.

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya