ZINAZOVUMA:

Polisi yazuia mikutano ya Bobi Wine Uganda

Jeshi la polisi nchini Uganda limezuia mikutano ya chama cha...

Share na:

Polisi nchini Uganda wamepiga marufuku mikutano ya kisiasa inayoandaliwa na kiongozi wa upinzani Robert Kyagulanyi, maarufu kama Bobi Wine, kutokana na ukiukaji wa utaratibu wa umma na kumchafua Rais.

Naibu Inspekta wa Polisi Tumusiime Katsigazi alisema kuwa mtu mmoja amefariki na wengine 10 walijeruhiwa vibaya katika mikutano ya chama hicho cha National Unity Platform (NUP).

Polisi pia wanamshutumu Kyagulanyi kwa kuchochea makundi katika mikutano yake iliyoanza siku ya Jumatatu.

Hata hivyo Kyagulanyi ameahidi kuendelea na mikutano na kuwataka wafuasi wake kusubiri ishara kutoka kwake.

Bobi Wine amekuwa akitumia mikutano hiyo kuinua uungwaji mkono na wananchi kabla ya uchaguzi mkuu wa 2026.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya