Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga amesitisha maandamano ambayo yaliyotarajiwa kuendelea siku ya leo na ataingia kwenye mazungumzo na serikali baada ya wiki mbili za maandamano kufanyika.
Toka kuanzishwa kwa maandamano hayo tarehe 20 machi zaidi ya watu watatu wamepoteza maisha yao na uharibifu wa baadhi ya maeneo ya biashara.
Maandamano hayo yanayoongozwa na Odinga ambae anamshutumu Raisi William Ruto kwa kufanya udanganyifu katika uchaguzi uliofanyika mwaka jana, amesitisha maandamano hayo na kuwa tayari kuzungumza na serikali.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya Raisi William Ruto kuomba kusitishwa kwa maandamano hayo na kuhitaji majadiliano ya wabunge wa pande zote mbili kushughulikia madai yao ikiwemo uteuzi wa kamishna wa Tume ya uchaguzi IEBC.