ZINAZOVUMA:

Rais Samia ampongeza Rais Mteule wa Senegal

Rais Samia ampongeza rais Mteule wa Senegal Bassirou Diomaye Faye...

Share na:

Rais Samia Suluhu Hassan amemuahidi ushirikiano wa karibu Rais mteule, Bassirou Diomaye Faye katika kuimarisha uhusiano na tija kwa pande zote za nchi hizo mbili.

Kupitia kurasa rasmi za mitandao ya kijamii za Rais Samia, ameandika, matarajio yake ni kuendelea kufanya kazi pamoja ili kuimarisha uhusiano ya nchi hizi mbili.

“Nawasilisha pongezi zangu za dhati kwa Mheshimiwa Bassirou Diomaye Faye, Rais Mteule wa Jamhuri ya Senegal, kwa ushindi wako katika uchaguzi wa urais wa 2024 wa Senegal; na watu wa Senegal kwa uchaguzi wa amani,” ameandika Amiri Jeshi Mkuu Samia Suluhu Hassan

Bassirou Diomaye Faye amekuwa rais mwenye umri mdogo zaidi nchini humo, akiwa na miaka 44. Amezaliwa Machi 25, 1980, katika jimbo la Thiès.

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya