ZINAZOVUMA:

Rais Samia kasema “Hakuna Kitakachosimama”

Kauli ya Rais Samia imetumka na Kamati ya Bunge ya...

Share na:

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya Ukimwi, Stanslaus Nyongo ameipongeza Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa kuendeleza miradi ya afya ambapo, ikithibitika kauli ya Rais Samia kuwa Hakuna mradi utakaosimama.

Nyongo amesema hayo leo Machi 16, 2024 baada ya kutembelea miradi ya ujenzi wa jengo la wodi la ghorofa mbili lenye uwezo wa vitanda 201 pamoja na jengo la mionzi yanayojengwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Chato akiambatana na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu.

katika kukazia maneno yale alitumia msemo wa Rais Samia kasema “Hakuna Kilichosimama” hivyo kamati wamethibitisha hilo baada ya kutembelea katika Hospitali ya Kanda ya Chato na kuona kasi ya ujenzi wa majengo hayo yanavyokwenda vizuri bila kikwazo chochote.

“Sisi kama Kamati tumeridhika baada ya kuona ujenzi unavyoendelea, tumeongea na wakandarasi wanapata fedha kwa wakati kwa hiyo tunampongeza sana Mhe. Rais Samia pamoja na Waziri wa Afya kwa kusimamia maendeleo haya,” Nyongo

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya