Nchi nzima ya Senegal iko roho juu wakingoja matokeo ya uchaguzi wa rais wa 2024. Wakati yakingojwa matokeo ya jumla tayari yameanza kutoka matekoe ya awali yanayoonyesha Diomaye akiongoza kwa asilimia zaidi ya 50.
Hii inaonyesha nchi imewaamini Diomaye na Sonko hadi wanapindua meza mbele ya chama tawala nchini humo.
Takwimu zilizokusanywa uwanjani na Alphonse Diombo Thiakane, mtaalamu wa takwimu wa Radio Futurs Médias (RFM), zimefunua mielekeo ya kwanza katika matokeo haya:
Bassirou Diomaye Faye: 56.13%
Amadou Ba: 31.4%
Khalifa Ababacar Sall: 4.0%
Aliou Mamadou Dia: 3.13%
Idrissa Seck: 1.6%
Inapaswa kuzingatiwa kwamba takwimu hizi zinawakilisha mielekeo ya awali na matokeo rasmi yatathibitishwa baadaye na mamlaka husika za uchaguzi.
Hata hivyo, ishara hizi za mapema zinaonyesha mandhari ya kisiasa inayobadilika na ushiriki mkubwa wa wapiga kura.
Mbali na mahakama mwezi Disemba kutoa amri ya Sonko kuwepo katika wagombea wa uchaguzi mwaka huu, hajaonekana katika wagombea na badala yake mwenzake amevuruga safu ya ulinzi ya chama tawala nchini Senegal.