ZINAZOVUMA:

NATO kununua ndege mpya za RADA

Nato kununua ndege za Rada mpya kama mpango wa kujizatiti...

Share na:

Umoja wa Kaskazini mwa Atlantiki – NATO unatarajia kubadili ndege inayotumika katika uchunguzi wa anga, ambayo imekuwa katika matumizi kwa zaidi ya miongo mine kuanzia mwaka 1980.

Umoja huo umetengeneza ndege aina ya Boeing 707 na kuifanya ya kijeshi kwa ajili ya kazi hizo.

Wanatarajia kununua ndege 6 zitakazofungwa vifaa mithili ya rada ili kuchunguza maeneo ya mbali na ndege hizo.

Ndege hizo mpya zina uwezo wa kuchukua taarifa kutoka umbali wa maili 250 sawa na kilomita 400.

Na pia zinaweza kuchukua taarifa katika eneo la kilomita laki 3 za (300,000sqKM) sawa na takriban maili laki na kumi na tano za mraba.

Moja huo unatarajia kuweka wino makubaliano ya kununua ndege hizo mwaka 2024, na kufungwa vifaa ili zianze kazi mwaka 2031.

Ndege za zamani zimesaidia misheni nyingi za NATO katika ukanda wa Balkan, Iraq na katika matukio mbalimbali kama kombe la dunia la 2006 nchini Ujerumani.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya