ZINAZOVUMA:

Ndege iliyowabeba wachezaji wa Arsenal yawaka moto.

Ndege iliyokua imebeba wachezaji wa timu ya wanawake ya Arsenal...

Share na:

Ndege iliyokuwa imebeba kikosi cha timu ya wanawake ya klabu ya Arsenal iliwaka moto siku ya jumapili usiku ilipokuwa ikirejea kutoka Ujerumani kwenye mchezo wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Wolfsburg.

Tukio hilo limetokea katika uwanja wa ndege wa Braunschweig, Wolfsburg baada ya kiumbe “ndege” kuingia ndani ya injini muda mfupi kabla ya kuruka na kusababisha kishindo kikubwa.

Mlipuko ulianza kutokea kwenye ndege hiyo aina ya Boeing 737 hali iliyopelekea marubani waliokuwa ndani ya ndege hiyo kuwahamisha haraka abiria, kikiwemo kikosi cha kwanza cha Arsenal, hadi mahali pa usalama.

Ikithibitisha kutokea kwa tatizo hilo Klabu ya Arsenal imesema kuwa wamerejea nyumbani salama leo mchana.

Taarifa hiyo imesema: “Ndege yetu ilipata tatizo la kiufundi kabla ya kupaa nchini Ujerumani Jumapili jioni na kutokana na hali hiyo tulibaki Wolfsburg usiku kucha wa jumapili kabla ya kuruka kurudi Uingereza Jumatatu mchana.
“Tungependa kuwashukuru wafanyakazi walio ndani ya ndege na walio chini kwenye uwanja wa ndege kwa usaidizi wao”

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,