ZINAZOVUMA:

ATCL yatangaza ujio wa ndege zingine nchini

Shirika la ndege la ATCL limesema mpaka sasa kuna ndege...

Share na:

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) Mhandisi Ladislaus Matindi amesema mwishoni mwa mwaka huu na mwanzoni mwa mwaka 2024, Serikali ya Tanzania itapokea ndege nyingine mpya tatu na kulifanya Shirika hilo kuwa na jumla ya Ndege 16.

Matindi amesema hivi sasa ATCL ina jumla ya ndege 13 zikiwepo ndege za Abiria 12 na moja ya mizigo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam leo Jumanne Agosti 15, 2023, Matindi amesema kati ya ndege hizo tatu zitakazowasili nchini, mbili ni aina ya Boeing 737 max 9, na moja ni aina ya Boeing 787.

Ndege hizo zinalenga kuboresha utolewaji wa huduma za usafiri kwa Watanzania na wageni lakini pia kurahisisha usafiri wa mizigo kutoka ndani na nje ya nchi.

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,