ZINAZOVUMA:

Majaliwa awataka wachunguzi wa Hesabu kuwa waaminifu

Waziri Mkuu wa Tanzania awataka wataalamu wa uchunguzi wa Hesabu...

Share na:

Waziri Mkuu wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amewataka wataalamu wa kamati za kuchunguza hesabu za serikali kuyatumia vyema mafunzo waliyopatiwa ili kuzuia mianya ya rushwa na kuongeza kasi ya uwajibikaji.

Waziri Mkuu amesema hayo Golden Tulip, Uuwanja wa Ndege Zanzibar wakati akifunga mafunzo ya kuwajengea uwezo wajumbe na wataalamu wa kamati ya SADCOPAC.

Amesema endapo wataalamu hao watayatekeleza kwa vitendo mafunzo hayo, wataweza kufanikisha malengo yaliyokusudiwa pamoja na kuleta mafanikio makubwa ya kiutendaji.

Aidha amesema, kuwa mafunzo hayo yatakuwa chachu kwa wajumbe kuweza kusimamia misingi ya uwajibikaji na kuimarisha haki na utawala bora.

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,