ZINAZOVUMA:

Waziri Mkuu: Azindua Kauli mbiu ya sherehe za Muunganao

Waziri Mkuu Kassim majaliwa azindua Nembo na Kauli mbiu ya...

Share na:

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amezindua Kauli mbiu na Nembo za sherehe ya miaka 60 ya Muungano.

Katika uzinduzi huo Waziri Mkuu awamewataka Watanzania wote Bara na Visiwani kudumisha, kujivunia, kuenzi pamoja na kuthamini muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Alisema kuwa muungano tulionao ni tunu adimu na adhimu na inapaswa kulindwa kwa gharama yoyote na kila mmoja achukue jukumu la ulinzi

Aidha Waziri Mkuu amesema watanzania wana kila sababu ya kujivunia muungano wao kutumiza miaka 60

“Ni ukweli usiopingika kwamba muungano wetu umeendelea kuwa na tija kubwa na kuchangia maendeleo ya nchi yetu na wananchi wote kwa ujumla” amesema Mh Majaliwa

Maadhimisho hayo ya miaka 60 ya Muungano yamebeba kauli mbiu isemayo “Miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Tumeshikamana na Tumeimarika, kwa maendeleo ya Taifa letu”

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,