ZINAZOVUMA:

Prof Mussa Assad: Hakuna uwajibikaji serikalini.

Aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali C.A.G...

Share na:

Aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad amedai hakuna uwajibikaji wa kutosha kutokana na mwendelezo wa ripoti zinazotolewa na idara hiyo kila Mwaka

Amesema “Mfano Ripoti ya Mwaka 2022 inaeleza kulikuwa na mapendekezo 205 yaliyotolewa Mwaka 2020, kati ya hayo 60% yamejibiwa, 40% hayakujibiwa. Inamaanisha kulikuwa na mapendekezo 82 hayakujibiwa na hatupewi taarifa yaliishiaje.”

Ameongeza “Mfano suala la kusema ‘Linaendelea kutekelezwa’ lina ukakasi, Ripoti inapotoka kunakuwa na Miaka miwili nyuma ya ukaguzi, hivyo jumla kunakuwa kama kuna Miaka mitatu hapo kati, sasa inakuwaje jambo linaendelea kutekelezwa kwa Miaka mitatu”.

Aidha Profesa Mussa Assad, ameshauri uwepo utaratibu wa kuwapa maumivu binafsi Wakuu wa Shirika au Wizara zinazosimamia Taasisi ambazo hazijatekeleza mapendekezo ya Ripoti ya C.A.G

Amesema “Mfano mshahara utapunguzwa kwa 5% mpaka 10% kila Mwezi, hiyo inamaanisha ikimalizika Miezi 10 hatakuwa na mshahara kabisa.”

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya