ZINAZOVUMA:

Lissu: Rushwa imekithiri uchaguzi wa ndani

Lissu ashangazwa watu kutumia pesa nyingi ili kupata vye ndani...

Share na:

Baada ya Lissu kutangaza jukwaani kuwa rushwa imekithiri kwenye uchaguzi wa ndani wa CHADEMA, hali iliyovuta hisia za wengi na kuleta taswira ya vita ya madaraka ndani ya chama.

Hii Imekuja wakati chama cha CHADEMA kipo katika maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za mitaa  na uchaguzi mkuu wa mwakani.

Lissu aliyatoa madai hayo katika Mkutano wa hadhara uliofanyika Mkoani Iringa, na kuibua sintofahamu kwa baadhi ya wanachama wa CHADEMA.

Huku baadhi ya wanachama wakihisi ni mgogoro wa maslahi na wengine wakihisi kuwa sababu ni vita ya kuteuliwa kuwania urais mwaka 2025 kwa tiketi ya chama hicho.
 
“kuna mtafaruku mkubwa sana wa uchaguzi ndani ya chama chetu, kuna pesa nyingi ajabu kwenye uchaguzi huu (ndani ya CHADEMA),” alisema.

Ambacho kimemshangaza zaidi ni kuambiwa na uongozi wa chama kuwa hakuna pesa za kufanya mikutano yake ya hadhara, lakini anashangaa kuona kuna pesa za rushwa kwenye uchaguzi wa ndani.

Kitendo cha Lissu kulalamika hadharani kuhusu rushwa ndani ya chama na kunyimwa pesa za maandamano na mikutano ya hadhara, kimetafsiriwa na baadhi ya Wanachadema kama ni utovu wa nidhamu na kukidhalilisha chama.

Wamedai kuwa utaratibu wa CHADEMA ni kuwa kiongozi huyo alitakiwa kuwasilisha malalamiko yake kwenye vikao rasmi vya ndani vya chama, ikiwemo Kamati Kuu, siyo jukwaani.

Mbowe na Lissu kwa nyakati tofauti wote  wamewahi kugombea urais mara moja na kushindwa na mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Na taarifa za ndani ya CHADEMA zinasema kuwa wote wanataka kugombea urais mwaka 2025, kupitia chama hicho mwaka na ndio sababu ya mtafaruku unaoendelea.

Pia inadaiwa kuwa Lissu amekuwa akifanya maandamano na mikutano ya hadhara, licha ya uongozi wa CHADEMA kumkataza Lissu asifanye hivyo hadi uchaguzi wa ndani umalizike.

Na katika mikutano yake Lissu amekuwa akiwataka wanachama wasiwachague viongozi wanaotumia pesa kama njia ya kupata madaraka kwenye uchaguzi wa ndaniwa CHADEMA.

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa nchini wanasema kuwa vita ya Mbowe na Lissu inatarajiwa kupamba moto zaidi siku zijazo, kwani mafahali hao wawili hawawezi kuishi kwenye zizi moja.

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,