ZINAZOVUMA:

Maandamano UVCCM yapigwa ‘stop’

Jeshi la polisi nchini limepiga marufuku maandamano yaliyokuwa yamepangwa kufanyika...

Share na:

Jeshi la Polisi nchini limepiga marufuku maandamano yaliyoandaliwa na Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) yenye lengo la kuunga mkono uwekezaji katika bandari.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na msemaji wa Jeshi hilo, David Misime jana Jumapili Julai 16, 2023 imesema maandamano hayo ya nchi nzima yatazua taharuki zisizo na msingi na badala yake hoja zote ziwasilishwe katika vyombo husika.

“Kwa msingi huo, Jeshi la Polisi linapiga marufuku maandamano hayo yasifanyike na hii ni pamoja na watu wengine wenye nia kama hizo na badala yake wawasilishe hoja zao kupitia mikutano na vyombo vya habari,” imesema taarifa hiyo iliyotolewa na Misime.

Aidha, Jeshi la Polisi limeongeza kuwa miongozo ya mtu au kikundi cha watu kinapotaka kuitisha maandamano ipo na inapaswa kufuatwa.

Taarifa hiyo ya Jeshi hilo lenye mamlaka ya kulinda raia na mali zao imekuja baada ya jana Jumapili Juni 16, 2023 Mwenyekiti wa UVCCM, Mohammed Kawaida kupitia vyombo vya habari kuhamasisha maandamano ya kuunga mkono Serikali katika uwekezaji wa bandari yaliyotarajiwa kufanyika Wilaya zote kuanzia Julai 18 mwaka huu.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya