ZINAZOVUMA:

LAM – Msumbiji yaibua ubadhirifu wa fedha

Shirika la Ndege la Msumbiji lakubali kudaiwa mafuta. Pia limeibua...

Share na:

Shirika la ndege la Msumbiji (LAM) limegundua ubadhirifu wa fedha kwa namna mbalimbali, uliosababisha hasara kwa shirika hilo.

Kurugenzi ya mabailiko ya Muundo wa shirika umegundua shirika hilo limekuwa likiuza tiketi nyingi za ndege, na fedha zinazoingia katika akaunti haziakisi kiasi hicho cha mauzo. Sérgio Matos Mkurugenzi wa kurugenzi hiyo alisema kuwa ili kujua ni wapi fedha hizo zinaenda, ilibidi wakusanye mashine zote za kuuzia tiketi.

Baadhi ya maeneo wamiliki wa maduka hawajui kuhusu uwepo wa mashine hizo za kuuzia tiketi na hawajui nani mmiliki wa mashinehizo. Uchunguzi huo ulioanza takriban wiki mbili zilizopita umegundua tofauti ya zaidi ya dola za marekani milioni 2 baina ya tiketi zilizouzwa na kiasi kilichoingia.

Pia uchunguzi huo umegundua kuna akaunti nchini Malawi yenye zaidi ya dola milioni 1 za marekani. Akaunti hiyo ya Malawi hakuna anayeweza kutoa pesa hizo wala kuzihamisha.

Pia uchunguzi huo umebaini kuwa kuna kughushi kwa taarifa za ujazaji wa mafuta kwenye ndege, kwani ndege ambayo inajaza mafuta tani 80 ilionekana kujazwa tani 95. Hii imesababisha maswali ya kuwa hizi tani 15 zimekuwa zikipelekwa wapi, bila kupata majibu kwa wakati huo.

Pia inaaminika kuwa kuna wafanyakazi ambao walikuwa wakitumia fedha za shirika hilo kujinunulia mali na nyumba zao binafsi.

Mali na mianya hiyo ya ubadhirifu ndani ya shirika hilo la ndege, pia aligusia na kusema kuwa ni kweli shirika hilo wanadaiwa mafuta. Ila alilitaja shirika la Petromoc pekee na kusema kuwa wanadaiwa na shirika hilo.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya