ZINAZOVUMA:

Yanga yaalikwa Malawi

Klabu ya Yanga imepata mualiko kutoka kwa Raisi wa Malawi...

Share na:

Klabu ya Yanga imealikwa na Rais wa Malawi, Lazarus Chakwera kuhudhuria sherehe za Uhuru wa Taifa hilo zitakazofanyika Julai 6, 2023 ambapo pia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan atahudhuria sherehe hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Leo Julai 3, 2023, Meneja Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ally Kamwe amesema kuwa wachezaji wote waliokuwa kwenye mapumziko wamekubali kuhudhuria sherehe hizo na Julai 5 wataondoka na Ndege Maalum wakiwa na wachezaji 15 kutoka Kikosi kikubwa na wengine 22 kutoka timu ya vijana ya U20.

Aidha Kamwe ameeleza kuwa siku hiyo ya Julai 5 Yanga watakuwa na hafla ya chakula cha Jioni na Rais wa Malawi.

Katika Sherehe hizo Yanga watacheza mchezo wa kirafiki na Timu ya Nyasa Big Bullets kutoka Malawi.

Ikumbukwe kuwa Malawi ilipata Uhuru wake Julai 6, 1964 miaka 59 iliyopita.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya