ZINAZOVUMA:

Kaunti ya Kilifi yapiga marufuku Mugoka

Siku chache baada ya Kaunti ya Mombasa kupiga marufuku biashara...

Share na:

Ofisi ya Gavana wa Kaunti ya Kilifi nchini Kenya imezuia kuingiza, kupitisha, kusambaza, kuuza pamoja na kutumia mirungi.

Hii itakuwa ni kaunti ya pili nchini humo kuweka zuio la biashara hiyo maarufu, baada ya kaunti ya Mombasa kuweka zuio la namna hiyo siku chache kabla.

Na kuzitaka biashara zote zinazojihusisha na mirungi katika kaunti yake, kufunga biashara zao mara moja au kuacha kuacha kujihusisha na mirungi.

Akaongeza kwa kuamrisha vyombo vya ulinzi na usalama kushughulika na hilo bila upendeleo wowote.

Gavana wa Kaunti ya Mombasa Abdulswamad Nassir alitoa tangazo kama lililotolewa na Gavana Mung’aro juu ya mirungi.

Na Gavana wa Kaunti ya Taveta Andrew Mwadime ameazimia kuweka zuio la biashara hiyo yenye mzizi wake kutoka kaunti ya Embu.

Wakati kaunti hizo mbili zikiweka zuio kabisa na Kaunti ya Taveta kuwa mbioni kuzuia, Kaunti ya Kwale imependekeza kuongeza kodi kwa wanaofanya biashara hiyo.

Hii ni baada ya wananchi kufikisha katika majukwaa ya maeneo mbalimbali kwenda kwa Gavana wa Kaunti ya Kwale Achani, awaongezee kodi.

Kwa sasa magari yanayobeba mirungi hutozwa shilingi elfu 10 ya Kenya, na badala yake wananchi hao wamependekeza magari hayo yatozwe laki 1 yanaypoingia Kwale.

Kaunti hizo za Pwani zimekuwa na msimamo mkali na tofauti dhidi ya Mirungi ambayo imezoeleka kutumika nchini Kenya kwa muda mrefu, kutokana na kuongezeka kwa watumiaji wake na wengi kuwa ni vijana wadogo.

Pia imeonekana kuna ongezeko la vijana wenye changamoto za afya ya akili kutokana na matumizi ya majani hayo, na kusababisha mzongo kwenye vituo vya afya kutokana na uraibu huo.

Miraa (au mirungi) ni majani na vitawi ya mrungi, na Mugoka ni majani machanga ya mmea huo. Miraa, Mirungi na Mugoka huy´tumika kama kichochezi (Dawa za kulevya) cha mwili na akili nchini Kenya, na pembe ya Afrika.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya