ZINAZOVUMA:

Mtoto wa Biden ashtakiwa kwa kutumia dawa za kulevya

Mtoto wa Rais wa Marekani anayeitwa Hunter Biden anashtakiwa kwa...

Share na:

Mtoto wa Rais wa Marekani Joe Biden anayeitwa Hunter Biden amefunguliwa mashitaka akituhumiwa kununua bunduki wakati akiwa ametumia dawa za kulevya aina ya cocaine.

Hunter Biden wakati anananua bunduki hiyo alidanganya kuwa hakuwa akitumia dawa za kulevya ili aweze kuuziwa silaha.

Mashitaka hayo dhidi ya Hunter mwenye umri wa miaka 53 yamezua mjadala mpya kwenye kampeni za urais wa Marekani mwaka.

Baba yake, Joe Biden anapanga kuwania tena urais wakati mpinzani wake mkuu wa chama cha Republican, Donald Trump akikabiliwa na mashitaka manne ya jinai, yenye jumla ya kesi 91 za kusikilizwa.

Mashitaka dhidi ya Hunter Biden hayakuwa yakitarajiwa, kwa kuwa mwongoza mashitaka maalum David Weiss alisema kwamba yangewasilishwa mwishoni mwa mwezi.

Aidha Wakili wa Hunter, Abbe Lowell amemshutumu muendesha mashtaka kwamba ameshinikizwa kisiasa na chama cha Republican katika kumfungulia mashitaka.

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya