ZINAZOVUMA:

Miili 901 yakutwa pwani ya Tunisia

Zaidi ya miili 901 imekutwa katika pwani ya Tunisia ya...

Share na:

Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Tunisia Kamel Feki amesema walinzi wa pwani ya nchi hiyo walipata miili 901 ya wahamiaji waliokufa maji kuanzia Januari 1 hadi Julai 20 mwaka huu.

Taifa hilo la Afrika Kaskazini linashuhudia wimbi kubwa la wahamiaji mwaka huu na majanga ya mara kwa mara ya kuzama kwa boti za wahamiaji kutoka nchi za Afrika, Kusini mwa jangwa la Sahara wakielekea kwenye pwani za Italia.

Tunisia imekua kama kituo kikuu cha kuanzisha safari kwa watu wanaokimbia umaskini na mizozo barani Afrika na Mashariki ya Kati kwa matumaini ya kuwa na maisha bora barani Ulaya.

Feki aliliambia bunge kwamba miongoni mwa miili 901 iliyopatikana, 36 ilikuwa ya Watunisia na 267 ya wahamiaji wa kigeni, huku uraia wa waliobaki ukiwa haujulikani.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya