ZINAZOVUMA:

Kamati ya Bunge yapongeza Serikali na TASAF

Kamati ya Bunge ya ya Utawala, Katiba na Sheria pamoja...

Share na:

Kamati ya Kudumu ya Bunge Utawala, Katiba na Sheria imeipongeza serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kupeleka fedha  katika miradi yenye tija Kwa  watu kupitia mfuko wa TASAF.

Kamati imetoa pongezi hizo baada ya kukagua mradi wa Stendi ya Mabasi Peramiho na soko la bidhaa mbalimbali la Madaba.

Akizungumza mbele ya wananchi Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Dk Joseph Mhagama  aliishukuru  serikali kwa miradi hiyo.

Miradi mingine iliyotembelewa na Kamati hiyo ya kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria ni Wodi ya Mama na Mtoto katika hospitali ya Kibena pamoja na mradi wa shamba la parachichi unaotekelezwa na walengwa wa TASAF katika kijiji cha Ibumilamkoani Ruvuma.

Mbali na shukrani za mwenyekiti wa kamati hiyo, pia Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mhe. Ridhiwani Kikwete alimshukuru Rais  Samia  kwa kuwezesha fedha kiasi cha Sh. Bilioni 1.5  kutekeleza miradi mbalimbali katika Mkoa wa Ruvuma pekee kupitia TASAF.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya