ZINAZOVUMA:

Spika Dkt.Tulia Aweka Historia, Ashinda Urais Wa Umoja Wa Mabunge Duniani-Amshukuru Rais Dkt.Samia, Asema Ana Deni Kwake

Dkt.Tulia amemshukuru sana Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa mchango wake...

Share na:

Anaandika Dkt.Ahmad Sovu

Tarehe 27/10/2023 Tanzania imeingia katika historia ya aina yake.

Ambapo Mheshimiwa Dkt.Tulia Ackson Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameshinda kwa kishindo nafasi ya kuwa mwanamke wa kwanza Mwafrika na Mtanzania kushika wadhifa huu mkubwa katika anga za dunia.👏👏👏.

Mwenyewe Dkt.Tulia amemshukuru sana Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa mchango wake na sapoti yake ilimsaidia kuibuka na ushindi huo mnono. Anasema ana deni kwa Mheshimiwa Rais Dkt.Samia kwa juhudi zake na serikali kufikia hatua hiyo.

Uchaguzi huo ambao umefanyika nchini Luanda, Angola katika mkutano wa jumuiya hiyo wa 147. Dkt.Tulia amechukua nafasi kutoka kwa Rais alomaliza muda wake Bwana Duarte Pacheko kutoka Portugal ambaye alichaguliwa tangu mwaka 2020.

Umoja wa Mabunge Duniani ni nini?

Umoja wa Mabunge Dunia ambao kwa Kiingereza hurejelewa kama Inter-Parliamentary Union yaani, IPU ni jumuiya ya kidunia iliyoanza tangu miaka ya 1889. Shabaha yake kuu ni kuhimiza, amani, demokrasia na maendeleo endelevu.

Takriban miaka 134 sasa, Umoja huo kwa sasa, utaongozwa na Rais Mteule Mwanamke, Spika wa Bunge la Tanzania. Kwa hakika hii ni jambo kubwa sana kwa nchi yetu na jumuiya ya Afrika Mashariki.

Kwa nini Spika Tulia?

Kwa hakika Spika Dkt.Tulia ameonesha uwezo na umahiri wenye uweledi kwa kiwango cha juu sana. Ameonesha upevu na ukomavu na ushiriki wake madhubuti katika kampeni kuhakikisha anashinda wadhifa huu muhimu. Hotuba yake wakati wa kuomba kura ilidhihirisha hayo.

Ushirikiano na uhusiano mwema wa Kimataifa ulichagizwa na Rais Dkt.Samia Suluhu katika kukuza Diplomasia ya kimataifa kwa hakika vimesaidia katika ushindi huu wa kishindo.

Ukuruba na uhusiano wa nemsi zake Dkt.Samia katika Jumuiya za Kikanda kama JAM, SADC na Umoja wa Afrika bila shaka vimekuwa chachu ya mafanikio katika ushindi huu.

Si jambo jepesi hata kidogo kuibuka na kura 172 kati ya kura 303 zilizopigwa na wajumbe kutoka nchi wanachama duniani kote.

Spika Tulia dhamira ileile ameibuka na kuwaacha kwa mbali washindani wenzake kama ifuatavyo:

  1. Adji Diarra Mergane Kanoute kutoka Senegal kura 54.
  2. Catherin Gotani Hara wa Malawi kura 61
  3. Marwa Abdibashir Hagi kutoka Somalia kura 11.

Na Mwamba mwenyewe 🤣🤣

  1. Dkt.Tulia Ackson kutoka Tanzania 🇹🇿 kura 173👏👏👏💪

Je, Nafasi hii ina maana gani kwa Tanzania?

Kwa hakika nafasi hii ni muhimu sana kwa Tanzania.

  • Inaonesha heshima kubwa kwa nchi yetu.
  • Inadhihirisha imani na heshima kubwa ambayo ipo kwa Tanzania kutoka kwa mataifa mbalimbali duniani. Mathalan, kwa Afrika tu nchi wanachama ni 52.
  • Imedhihirisha juhudi kubwa anazozifanya Mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan za kuitangaza nchi yetu Kimataifa lakini na kupambania diplomasia ya kiuchumi kwa nchi yetu.
  • Itaongeza chachu ya kukuza demokrasia katika mabunge yetu na kulinda amani katika nchi hizi.
  • Itaendelea kuitangaza nchi yetu Kimataifa zaidi.Italeta fursa mbalimbali zitokanazo na jumuiya hii bila shaka Tanzania na Afrika Mashariki tunafaika nazo zaidi.
  • Kuendelea kumpa heshima na nafasi yake mwanamke wa Afrika.
  • Inaendelea kukuza na kujenga kujiamini kwa wanawake na Watanzania wote kwa ujumla katika kupambania nafasi hizi katika anga za kimataifa.
  • Inaamsha ari na bidii katika kazi n.k

Amshukuru Rais Dkt.Samia na kuonesha upevu baada ya Uchaguzi

Katika hotuba yake, mara baada ya shughuli ya uchaguzi kuisha. Dkt.Tulia Ackson Rais mpya wa IPU alionesha ukomavu na upevu wa hali ya juu.

Kwanza, alimshukuru sana Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa sapoti yake kubwa. Baada ya hapo aliwashukuru wagombea wenzie wote kwa kuonesha ushindani katika kinyang’anyiro hicho.

Mbali ya kuwashukuru kwa chachu ya ushindi huu, pia alieleza kuwa atashirikiana nao ipasavyo katika mipango na ndoto zao za kuiendeleza jumuiya hiyo.

Kwa hakika nasi tunaungana na Mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kumpongeza Dkt.Tulia Ackson Mwansasu kwa kutwaa wadhifa huu muhimu.

Ni matumaini yetu kuwa utaonesha uweledi na umahiri wa hali ya juu katika kutimiza wajibu wako huu. Kongole pia, kwa timu yote ya Kampeni. Walau Umajumui wa Kiafrika tumeushuhudia katika mkutano huu.

sovu82@gmail.com

Endelea Kusoma

Uchambuzi wa Maeneo ma 3 muhimu ya Kitajriba katika uteuzi huu wa

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya