Rais Samia Suluhu Hassan amezindua Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini Mtwara.
Hospitali hiyo itahudumia wagonjwa wa rufaa kutoka mikoa ya Mtwara, Lindi, Ruvuma, na nchi jirani kama Msumbiji, Zambia, Malawi, na visiwa vya Comoro.
Hospitali hiyo yenye ghorofa tano, imegharimu takribani bilioni 15 katika ujenzi wake hadi kukamilika.
Inakadiriwa kuwa hospitali hiyo itakuwa na uwezo wa kuhudumia wagonjwa 800-1,000 na uwezo wa kulaza wagonjwa 1000.
Huduma zitakazotolewa hospitalini hapo ni pamoja na upasuaji wa Jumla, tiba (Internal Medicine), matibabu ya moyo, matibabu ya watoto, tiba ya uzazi na via vya uzazi (Obstetrics and Gynaecology).
Aidha Rais Samia atakagua na kuzindua miradi mbalimbali mkoani Mtwara katika ziara yake.