ZINAZOVUMA:

HAMAS yataka mapigano yasitishwe Gaza

Hamas yataka mashambulizi yanayoendelea kuporormoka Gaza yasitishwe, kama kipengele katika...

Share na:

Baada ya Hamas na Israel kufikia makualiano ya kubadilishana mateka wa pande mbili, waliotekwa kipindi cha mashambulizi ya Ukanda wa Gaza.

Hamas inasisitiza kuwa makubaliano yoyote ya kubadilishana mateka na Israel, lazima yajumuishe usitishaji wa kudumu wa mashambulizi huko Gaza, alisema Mkuu wa Ofisi ya Uhusiano wa Kimataifa wa Kundi hilo.

Katika mahojiano na kituo cha televisheni cha Al-Aqsa, Mousa Abu Marzouk alisema kutakuwa na mkutano wa makundi ya Wapalestina nchini China na wanatumai kuwa utamaliza mgawanyiko wowote.

Kuhusu mazungumzo kati ya Hamas na Israel kwa ajili ya makubaliano, Abu Marzouk alisema “upinzani unasisitiza kwamba makubaliano hayo ni pamoja na usitishaji wa kudumu wa vita.”

“Tunatafuta kujumuisha Urusi, Türkiye na China kama wadhamini kwenye mazungumzo hayo” alisema.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya