ZINAZOVUMA:

Watoa misaada Gaza washambuliwa na Israeli

Shirika la World Central Kitchen Gaza limeshambuliwa na moja ya...

Share na:

Habari kubwa kuhusu vita inayoendelea Gaza kati ya majeshi ya Israeli (IDF) na Hamas ni kuwa ndege ya kivita imewashambulia wafanyakazi wa shirika la misaada linaloitwa World Central Kitchen. Wafanyakazi waliokufa ni kutoka mataifa mbalimbali. Australia, Poland, UK na mwingine mwenye uraia pacha wa US na Canada. Mmoja uraia wake haujajulikana na waliobakia ni raia wa kipalestina.

World Central Kitchen ni shirika la misaada liliopo Marekani na Kiongozi wake Chef Jose Andres amekemea vikali tukio hilo kwenye mtandao wa twitter au X kwa kwa kuwaasa Israeli kuacha kuwashambulia wananchi na kutumia njaa kama silaha ya kivita. WCK imeenda mbali zaidi kutishia kusitisha huduma zake za misaada Gaza kama mataifa mbalimbali yatashindwa kuwahasa Israel kulinda wafanyakazi wanaotoa huduma za misaada.

Israeli imesema kuwa inafanya uchunguzi wa hali ya juu kuhusu swala hilo na kutoa ripoti kamili. Wadau wengi wakiona kama uchunguzi huo ni njia ya kuwapa msala Hamas kwa tukio hilo. Serikali ya Australia imekuwa serikali ya kwanza kuonesha hasira yake na waziri mkuu wa nchi hiyo akitaka waliohusika wakamatwe na Israeli kutoa majibu stahiki.

Shambulio hilo linazidi kuleta utengano kati ya Israeli na mataifa shirika kwani waliokufa ni kutoka mataifa ambayo yanaikingia kifua Israel kwenye hii vita.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya