ZINAZOVUMA:

Korea Kaskazini waficha genge la wadukuzi

Genge la wadukuzi lawazidi ujanja wamarekani na kuiba fedha za...
Kim Jong Un
Raisi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un akihutubia wananchi wa taifa lake

Share na:

Genge la wadukuzi linaloaminika kufadhiliwa na serikali ya Korea Kaskazini, limedukua kampuni mbalimbali zinazohusika na fedha za mtandaoni (cryptos).

Genge hilo llitumia kampuni ya kusimamia mifumo ya kompyuta kama daraja la kufikia kampuni hizo za fedha za kimtandao.

Wadukuzi hao walidukua kampuni ya JumpCloud ya mjini Colorado na kuiba fedha za kimtandao.

Baada ya tukio hilo kampuni ya JumpCloud ilishirikiana na kampuni ya CrowdStrike kufanya uchunguzi. Taarifa za uchunguzi zinaonyesha kuwa genge la wadukuzi la “Labirynth Chollima”, lenye uhusiano na Korea Kaskazini ndio limefanya udukuzi huo.

Sababu inayotazamiwa kufanya dukuzi kama hizi, ni kutengeneza fedha kwa ajili ya taifa hilo la Korea Kaskazini.

Udukuzi huo pamoja na wizi unaoaminika kufanyika mwishoni mwa mwezi Juni, ulithibitishwa na kampuni ya JumpCloud kwa chapisho katika blogu yake.

Ila haikusema chochote juu ya nani katika wateja wake ndio walioathirika na udukuzi huo.

Hata hivyo, ujumbe maalumu wa kutoka nchini Korea Kaskazini haujasema chochote juu ya udukuzi huo.

Na hapo awali nchi hiyo ilikana kuhusika kwake licha ya ushahidi lukuki kuonyesha uhusika wao.

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,