ZINAZOVUMA:

Serikali kufanyia kazi ripoti ya C.A.G.

Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa amesema serikali tayari imeanza kufanyia kazi...

Share na:

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema serikali tayari imeanza kuifanyia kazi taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali ya mwaka baada ya kuwasilishwa rasmi Bungeni Aprili 6, mwaka huu.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo jana (Alhamisi, Aprili 13, 2023) wakati akihitimisha hoja zilizotolewa na wabunge wakati wakijadili mwelekeo wa kazi za serikali na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2023/2024.

Aidha Waziri Mkuu amezielekeza Halmashauri zote nchini kusitisha utoaji wa fedha za mikopo zitokanazo na asilimia 10 ya makusanyo ya Halmashauri kwa makundi maalum ya vijana, wanawake na wenye ulemavu kuanzia Aprili hadi Juni, 2023 wakati Serikali inajipanga kuweka mfumo mpya wa utoaji wa mikopo hiyo.

Pia amemtaka Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, kuhakikisha kuwa Maafisa Manunuzi kwenye Halmashauri hawawi kikwazo katika kufanikisha utekelezaji wa vipaumbele vya matumizi ya Fedha za Mfuko wa Jimbo hususan upatikanaji wa vifaa kwa mujibu wa Sheria ya Manunuzi ya Umma.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya