ZINAZOVUMA:

ZAECA kutaifisha mali zote ukikutwa na uhujumu uchumi zanzibar

Mkurugenzi Mkuu ZAECA (ZAECA) Zanzibar Ali Abdallah Ali ,amesema mamlaka...

Share na:

Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya kuzuiya rushwa na uhujumu uchumi zanzibar (ZAECA) Ali Abdallah Ali ,amesema mamlaka iyo iko njiani kurudisha fedha zilizotokana uhalifu ikiweko rushwa na uhujumu uchumi ambapo mamlaka iyo itapora mali zote endapo utabainika kwa maswala ya uhujumu uchumi.

Ameyasema hayo wakati wa mafunzo wa watendaji wa ZAECA na wafanyakazi wa Tasisi mbali mbali za serikali Baada ya kupatiwa mafunzo hayo na ACFE Inayojishughulisha na maswala ya rushwa na uhujumu uchumi Tanzania.

” Tupo katika hatu ya kurejesha fedha ambazo zimetokana na madhalia ya uhalifu ikiwemo makosa ya rushwa,uhujumu uchumi ,ubadhirifu utakatishaji wa fedha haramu na makosa mengine ,tunazo mali zao mbali mbali magari ,nyumba ,viwanja tunavidhibiti andapo kesi tumeshinda mahakamani tunaiyomba mahakama kuchukua mali zote zilizotokana na uhalifu na kurudi serikali” — Ali Abdallah Mkurugenzi ZAECA.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya