ZINAZOVUMA:

‘Toto Afya ilihatarisha uhai wa Bima ya Afya’

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema kifurushi cha Toto Afya...

Share na:

Serikali imebainisha kuwa ililazimika kufuta kifurushi cha Toto Afya Card kufuatia tathmini waliyofanya na kuona kifurushi hicho kinahatarisha uhai wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF).

Hayo yameelezwa leo Bungeni na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu wakati akijibu hoja za Wabunge waliochangia makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2023/24 na kusema kuwa asilimia 70 ya fedha za hospitali za uma na binafsi zinategemea NHIF

“Bima ya Afya ndio roho ya huduma za afya nchini. Tumefanya utafiti na kuona baadhi ya vifurushi vinahatarisha uhai na uendelevu wa mfuko wa bima ya afya,” amesema Waziri Ummy.

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,