ZINAZOVUMA:

Watu 8 wafariki baada ya lori la mafuta kulipuka

Watu nane wamefariki baada ya lori lililobeba mafuta kuanguka pembezoni...

Share na:

Takriban watu 8 wamethibitishwa kufariki baada ya kutokea mlipuko wa lori la mafuta katika jimbo la Ondo Kusini Magharibi mwa Nigeria.

Mlipuko huo ulitokea baada ya wakazi wa eneo hilo kuchota mafuta kutoka kwenye lori lililopata ajali ya barabarani usiku wa Jana jumapili.

Kamanda wa polisi wa jimbo la Ondo amesema lori lililokuwa limepakia mafuta lilianguka pembezoni mwa barabara, na mafuta karibu yote yalimwagika huku wakazi wa eneo hilo wakikimbilia kuchukua mafuta.

“Lori hilo la mafuta lililipuka lenyewe na kuua watu 8 huku wengine wengi wakijeruhiwa ambao kwa sasa wanatibiwa hospitalini” msemaji wa Polisi alisema

Wakaazi na walioshuhudia tukio hilo wanasema lori hilo lililipuka katika mtaa ulio karibu na kituo cha mafuta na jengo la kanisa lakini mlipuko huo haukuleta madhara katika maeneo hayo.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya