ZINAZOVUMA:

Geita: Kijana afariki akichimba kaburi

kijana wa miaka 25 aliyekuwa akichimba kabri mkoani Geita wilaya...

Share na:

Kijana aliyefahamika kwa Majina ya Peter Simoni (25) Mkazi wa mtaa wa Mkoani Halmashauri ya Mji Geita Mkoani Geita amefariki Dunia ghafla wakati akishirikia na wenzake katika kuchimba kaburi la Marehemu Bi. Elizabeth Kalamu Mkazi wa Eneo la Mkoani.

Akizungumza Mmoja wa Mashuhuda waliokuwepo katika eneo la Tukio aliyefahamika kwa Jina la Bw. Paschal Charles ambaye pia walikuwa wakishirikiana katika kuchimba kaburi hilo amesema ulifika muda wa kupumzika kijana huyo ndipo aliambiwa atokea kabla hajatoka ndani ya kaburi hilo alianguka chini na kufariki Dunia.

” kwa kweli huyo kijana tunaishi naye mji mmoja unaona badaye huyo kijana akaingia kuchimba alivyoingia kuchimba akachimba kwa muda mfupi sana kama tunavyo pokezanaga yule kijana alivyoambiwa tokamo na wewe yule kijana ghafla kama kitu kilimshika akaishiwa nguvu kwa haraka tulikuwa pale tukajua labda yule kijana ana tatizo la kifafa tukamtoa tukamuweka nje kidogo pembeni siye tukaambizana bana tuendele huwenda huyu ana tatizo la kifafa kwa dakika kadhaa tu yani kitu kama dakika moja yule kijana kwenda kumwangalia kashabadilika, ” Paschal Charles.

Dkt. Thomas Mafulu ni Kaimu Mganga Mfawidhi Hospitali ya Halmashauri ya Mji Geita amethibitisha kifo hicho huku akisema kijana huyo alikumbwa na shambulio la Moyo lililopelekea kupoteza Maisha .

“Mwenzetu alikumbwa na shambulio la Moyo (Heart Attack) linaweza pelekea mtu kupoteza maisha kama akiwa mbali na wataalamu wa kumsaidia tunashauriwa tukipata tukipata na hiyo hali maana habari zake kuu pale imetokea ghafla mtu anapata maumivu makali ya kifua hasa hasa upande wa kushoto yanakuwa yanaambatana na kifua kubana kwahiyo inapelekea anashindwa kufanya chochote, ” Dkt. Mafulu.

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya