ZINAZOVUMA:

JKCI kuwa hospitali kubwa ya moyo Afrika

Serikali ya China imesema itaongeza msaada wa kifedha kwa taasisi...

Share na:

Serikali ya China imesema itaongeza msaada wa kifedha kwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) ili kuiboresha na kuifanya kuwa kitovu kikubwa cha matibabu ya moyo barani Afrika.

Akizungumza huko Beijing akiwa na Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba Mwenyekiti wa Shirika la Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa la China (CIDCA), Luo Zhohui amesema msaada huo utajumuisha ujenzi wa majengo ya kisasa, ufungaji wa vifaa vya matibabu ya kisasa, na mafunzo.

Wawili hao wamekutana kwa muda mfupi wakati wa ziara ya kikazi ya Dkt. Mwigulu nchini China huku wakiahidi kuendelea kukuza ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

Ushirikiano kati ya China na Tanzania umekuwa ukiongezeka katika maeneo mbalimbali. China imekuwa ikiisaidia Tanzania kwa kutoa misaada ya kifedha na miradi ya maendeleo, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa miundombinu, huduma za afya, elimu, teknolojia, kukuza utalii na utamaduni, biashara, uwekezaji, na ushirikiano wa kiuchumi.

Ushirikiano huu unalenga kuleta faida kwa pande zote na kuchangia maendeleo endelevu na ushirikiano wa kirafiki kati ya China na Tanzania.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya