ZINAZOVUMA:

Dkt. Nchimbi: Waambieni kazi za maendeleo zinazofanywa

Dkt. Nchimbi awataka viongozi wa kuwaambia wananchi kazi za kimaendeleo...

Share na:

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Dk Emmanuel Nchimbi, amewataka viongozi mbalimbali nchini kuwa na utaratibu wa kuwataarifu wananchi juu ya kazi za kimaendeleo zinazofanywa na Serikali.

Na kuendelea kusema kuwa ikiwa viongozi hao watakuwa na kawaida ya kusema kazi hizo za maendeleo itapunguza maswali ya wananchi juu ya utendaji wa serikali yao.

Ameyasema hayo akiwa katika ziara yake ya kwanza mkoani Katavi alipokuwa akitoa salam za Chama katika ofisi ya CCM mkoa.

katika salamu hizo alitoa tahadhari ya kutosikiliza kero ambazo kesi zake zinaendelea mahakamani.

Dk Nchimbi tayari ameanza ziara yake mkoani Katavi, na baada ya hapo atatembelea mikoa mingine mitano ili kukamilisha ziara yake ya mikoa sita.

Ziara ya Dkt. Nchimbi inatarajiwa kuwa katika mikoa ya Katavi, Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Ruvuma.

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,