ZINAZOVUMA:

Serikali iterejesha miundombinu ya barabara Rukwa

Share na:

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema Serikali imejipanga kuhakikisha inarejesha miundombinu ya barabara ya Kasansa hadi Kilyamatundu yenye kilomita 180.

Barabara hiyo iliyoathiriwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha maeneo tofauti tofauti nchini.

Bashungwa ameeleza hayo Aprili 08, 2024 Mkoani Rukwa wakati akikagua barabara hiyo na kuwahakikishia wananchi kuwa Serikali itafanya matengenezo makubwa katika maeneo korofi

Maeneo ambayo serikali itaongeza nguvu kutokana na ukorofi wake ni Nkwilo, Mtowisa, Zimba, Kisa, Kinambo, Ilemba na Solola ambayo yameathiriwa kwa kiasi kikubwa.

“Niwaahidi wana Rukwa, Serikali itaendelea kufanya kila jitihada kurejesha miundombinu katika maeneo yaliyoharibiwa na mvua kadri inavyowezekana ili huduma za kijamii na kiuchumi ziweze kuendelea kama kawaida”, amesema Bashungwa.

Aidha, Bashungwa amesema Wizara ya Ujenzi italeta wataalam wa miamba ili kutafiti Mlima Ufipa hasa eneo la Nkowilo.

Nkowilo imekuwa imetokea changamoto ya mawe mengi kushuka kutokea Milimani, tafiti hiyo itasaidia kupata chanzo cha tatizo hilo na hata suluhisho la kudumu katika miundombinu iliyopo katika Bonde la Ziwa Rukwa.

Kutokana na ombi la Mbunge wa Jimbo la Kwela, Deus Sangu la kuomba la kuunganisbwa kwa barabara ya eneo la Muze kuelekea Sumbawanga na barabara ya Ilemba kuuganishwa na Mkoa wa Songwe, Waziri Bashungwa amesema Serikali inepokea ombi hilo na italifanyia kazi.

Pia Waziri awapongeza Mkurugezi wa Matengenezo wa TANROADS, Dkt. Christina Kayoza pamoja na Mameneja wa Mikoa wa TANROADS kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kuhakikisha wanarejesha miundombinu ya barabara kwa haraka pindi inapoharibiwa na mvua.

Vilevile, Bashungwa ametoa wito kwa wananchi na waendesha vyombo vya moto kuchukua tahadhari katika kipindi hiki cha mvua za El-Nino, pale wanapokuta barabara au madaraja yamejaa maji waweze kusimama na kusubiri yapungue ndipo wapite.

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya